Russia is waging a disgraceful war on Ukraine.     Ukrayna'nın Yanında Olun!
  • Tanzania, Nakupenda Kwa Moyo Wote

  • 2 çeviri
    İngilizce #1, #2
Paylaşmak
Yazı tipi boyutu
Orijinal şarkı sözleri

Tanzania, Nakupenda Kwa Moyo Wote sözleri

Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania
Jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo ni heri mama wee
Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.
 
Tanzania, Tanzania
Ninapokwenda safarini
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania, Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.
 
Tanzania, Tanzania
Watu wako ni wema sana
Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena
Na wageni wa kukimbilia ngome yako imara kweli wee
Tanzania, Tanzania
Heri yako kwa mataifa.
 
Tanzania, Tanzania
Karibu wasio na kwao
Wenye shida na taabu
Kukimbizwa na walowezi
Tanzania yawakaribisha
Tuungane kiume chema wee
Tanzania, Tanzania
Mola awe na we daima.
 

 

"Tanzania, Nakupenda ..." çevirileri
İngilizce #1, #2
Yorumlar