• MwanaFA

    Dume Suruali

    Featuring artist: Vanessa Mdee
Favorites
Share
Font Size
Original

Dume Suruali lyrics

Vanessa Mdee
We ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
 
Hudat hudat hii ni salam na ufahamu
Kama unauza mapenzi siyo kwa binamu
Huna haja ya kusubiri hii ni hukumu
Hakuna kitu utapata utangoja kama askari wa zamu
Dume suruali, dume kaptula
Shauri zako ilimradi sipati hasara
Usione utani me sihongi hata kwa ishara
Utaniambia nini mpaka unigeuze fala
Kwanza nasikia hongo zinaleta mkosi...
Sentano yangu hugusi hata ukiongea kidosi
Yabaki mapenzi tusileteane ujambazi
Hata upige sarakasi utachonga viazi
(Bahili kama nini!)
Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada, hunitakii mema
 
Vanessa Mdee
We ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
I want that Gucci, Fendi, spend it on a girl like me
My name is Vee Money, money, spend it on a girl like me
 
Nihonge nanunua nini kwa nini yaani!
Kuna kipi nisichokijua ina TV ndani?
Usiulize n’takupa nini dada piga moyo konde
Viuno vingi kama mwali wa kimakonde
Usipende hela kama mfuko
Au fanya unavyofanya upate zako
Vishawishi vingi binti sema na moyo wako
Na ujifunze pesa zinauza utu wako
Tajiri mtata kama Salah
Zipo ila sitoi sobe hili me ni balaa
Unapenda hela zangu nami nazipenda pia
Kila mtu abaki na zake bye baby, tutaongea
(Mwanaume wa hivyo wa nini sasa!)
Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada, hunitakii mema
 
Vanessa Mdee
We ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
I want that Gucci, Fendi, spend it on a girl like me
My name is Vee Money, money, spend it on a girl like me
 
Aje aje ajee me mtoto fulani ghali
Nihonge gari, ma sweet sweet baby
Wanna see you today, unipeleke party
Aje aje ajeee njoo nikupe TBT
 
Siyo kwa enzi ya Magufuli
Zali ilikuwa long siku hizi hakuna la mentali
Nikikuhonga na ukiniacha nitakujia usingizini
Naepusha shari matatizo yote ya nini
Hakuna kipya chini ya jua
Hata nisiyoyafanya nishayasikia
Ningekuwa mhongaji ningeshafulia wangu
Mademu wangu wa zamani wote wangekuwa maadui zangu
(Mwanaume hovyo wewe!)
Ndiyo mnavyosema
Na ukiniomba kesho hunisikii tena
Kwani unauza nini dada, hunitakii mema
(Baki na hamu zako!)
 
Vanessa Mdee
We ni dume suruali kaa mbali nami, mbali nami
Kama dume suruali kaa mbali nami, uendani nami
I want that Gucci, Fendi, spend it on a girl like me
My name is Vee Money, money, spend it on a girl like me
 
[Vanessa] Baba bure huyu!!!
[MwanaFA] Hata pantoni lina staff
[Vanessa] Unamwambia nani sasa!
Unamwaaambia nani sasa!
 
MwanaFA: Top 3
Please help to translate "Dume Suruali"
Comments